FIQH ni neno la kiarabu lenye maana mbili. Maana ya kwanza ni ya kilugha na ya pili ni ya kisharia. Katika lugha ya kiarabu neno "FIQH" maana yake kufahamu/kujua.
FIQH: kwa mtazamo wa sheria ni fani ya elimu inyoshughulikia na kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na na taratibu za Uislamu katika maisha ya kila siku kwa ujumla fiqh ni sheria zinazoyatawala maisha ya Muislamu katika nyanja zote za maisha, kuanzia elimu, ibada, uchumi, ulinzi na usalama, ndoa, mirathi N.k.
MISINGI YA FIQ-HI
Misingi ya fiq-h ni chimbuko la elimu hii yaani mahala ambamo elimu hii imechukuliwa. Elimu ya fiqh imejiegemeza katika misingi mikuu minne
1.Qur-ani
2. Hadithi(sunnah)
3.Ijmaa
4.Qiyaasi
Hii ndio misingi na tegemeo la elimu hii ya fiqh.
Wamekubaliana wanawachuoni wote wa Fani hii ya Elimu ya Fiqh Juu ya Misingi Mikuu Miwili yanii Qur - an na Hadith (Sunnah) Na wametofautiana katika baki ya Misingi.
MAJINA YA MAIMAMU WAKUU WANNE KATIKA ELIMU YA FIQH
1.IMAMU ABUU HANIFA NU3MAAN
2.IMAMU MAALIK
3.IMAMU SHAFIIH
4.IMAMU AHMAD IBN HANBAL
No comments:
Post a Comment