Tuesday, 4 April 2017

Umuhimu wa kuswal Jama'ah





Anas Ibni Malik (Radhiallahu Anhu) amesema kuwa, Rasulullahi (Swallallahu Alaihi Wasalam) amesema:

"Mtu atakaeswali kwa ajili ya kutaka radhi za Allah, kwa muda wa siku arobaini kwa jamaa na huku anapata Takbira ya kwanza, huandikiwa kuepushwa na mawili. Kuepushwa na moto wa Jahannam, na kuepushwa na unafiki."

Maelezo:- Ikiwa mtu atadumu kuswali kwa Ikhlas, kwa muda wa siku arobaini na anaunga jamaa kutoka mwanzo, yaani Imamu asomapo Takbira ya mwanzo, huyu hawezi kuwa mnafiki, na wala hawezi kwenda Jahannam. Mnafiki ni mtu anaedai kuwa Muislam hali ya kuwa kuna "Kufru" moyoni mwake.

Kuanza kuumbwa mwanadam, huchukua kipindi cha siku arobaini akiwa tone la dam. Siku arobaini pande la nyama, na huendelea kubadirika, kila baada ya siku arobaini. Hii ndio sababu Masufi huutilia umuhimu sana muda huu uitwao "Chilla" katika lugha ya "Kiurdu", kwa ajili ya maendeleo ya kiroho.

Wamebahatika sana, watu ambao haiwapiti Takbira ya mwanzo mfululizo kwa muda wa miaka kadhaa.

Tujitahidi sana kuziwahi takbira za mwanzo wa Swala ili tuepushwe na hayo Aliyotuahidi muumba wetu.

No comments:

Post a Comment