Wednesday, 3 May 2017

JE IMEPENDEKEZWA KUFUNGA SHAABAN YOTE?



🌴💥هل يستحب الصيام شعبان كله ؟؟ 💥🌴

JEE IMEPENDEKEZWA KUFUNGA SHAABAN YOTE........??

✍عن أم سلمة رضي الله عنها قالت: ما رأيت رسول الله صلى الله عليه وسلم صام شهرين متتابعين إلا أنه كان يصل شعبان برمضان.

📚سنن أبى داود/٢٣٣٦.
📚سنن النسائى/٢١٧٥.
📚سنن ابن ماجه/١٦٤٨.
📚مسند لإمام أحمد/٦٢٥٢٢.

✍Kutoka kwa Ummu Salamah Allaah amridhie amesema: Sijamuona Mtume swalla llaahu alayhi wasallam akifunga miezi miwili ikifuatana isipokuwa alikuwa akiunganisha Shaaban kwa Ramadhan.

📚SUNAN ABI DAAUD/2336.
📚SUNAN AN-NASAAI/2175.
📚SUNAN BNU MAJAH/1648.
📚MUSNAD ya Imaam Ahmad/62522.

🖌🖋واللفظ لأبي داود:
أن النبي صلى الله عليه وسلم لم يكن يصوم من السنة شهرا تاما إلا شعبان يصله برمضان.

📚صحيح أبو داود/٢٠٤٨.

🖌🖋Na matamshi ya Tirmidhi:
Hakika Mtume swalla llaahu alayhi wasallam alikuwa hafungi katika mwaka mwezi mzima isipokuwa Shaaban akiunganisha na Ramadhan.

📚SAHIH TIRMIDHI/2048.

✍عن أبي سلمة رضي الله عنه قال: سألت عائشة رضي الله عنها عن صيام رسول الله فقالت: كان يصوم حتى نقول قد صام ويفطر حتى نقول قد أفطر. ولم أره صائما من شهر قط أكثر صيامه من شعبان كان يصوم شعبان إلا قليلا.

📚صحيح مسلم/١١٥٦.

✍Kutoka kwa Abi Salamah Allaah amridhie amesema: Nilimuuliza Aisha Allaah amridhie kuhusu funga ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallam akasema: Alikuwa akifunga mpaka twasema kwa hakika amefunga {{kwa wingi wake}} na alikuwa akila mpaka twasema kwa hakika amekula {{kukaa sana bila ya kufunga}}. Na Sijamuona akifunga mwezi kwa wingi ila Shaaban alikuwa akifunga yote  isipokuwa kwa uchache ((ila siku chache)).

📚SAHIH MUSLIM/1156.

🔴ذهب جمهور من العلماء إلى أن النبي صلى الله عليه وسلم لم يكن يكمل صيام شهر إلا رمضان.

==إما كلمة كله==
قالوا: وهذا جائز  في اللغة إذا صام الرجل أكثر الشهر يقال صاه الشهر كله.
 قاله الشوكاني في نيل الأوطار.

🔴Wamesema wanachuoni kuwa Mtume swalla llaahu alayhi wasallam hajawahi kumaliza kufunga mwezi ila Ramadhan.

Ama neno==YOTE==
wanasema wanachuoni  hii inafaa katika lugha atakapo funga mtu mwezi kwa wingi anaambiwa amefunga mwezi mzima.

Ameyasema maneno haya Imaam Ash-shawkaany katika kitabu NAILUL AWTHWAAR.

🌴🌴قال النووي رحمه الله:
==كان يصوم شعبان كله اي غالبه.
Amesema Imaam An-Nawawiyy Allaah amrehemu:

==Alikuwa akifunga yote maana yake "saana"

🌱🌱.......MTUME HAKUFUNGA SHAABAN YOTE KWA DALILI HIZI......🌱🌱

✍عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: ما صام النبي صلى الله عليه وسلم شهر كاملا قط غير رمضان.

📚صحيح البخاري/١٩٧١.
📚صحيح مسلم/١١٥٧.

✍Kutoka kwa Ibn Abbaas Allaah amridhie amesema: Hajafunga Mtume swalla llaahu alayhi wasallam mwezi kamili ila Ramadhan.

📚SAHIH BUKHAARI/1971.
📚SAHIH MUSLIM/1157.

✍عن عائشة رضي الله عنها قالت: ولا أعلم نبي قرأ القرآن كان في ليلة ولا صلى ليلة إلى الصبح ولا صيام شهر كاملا غير رمضان.

📚صحيح مسلم/٧٤٦.

✍Kutoka kwa Aisha Allaah amridhie amesema: Na wala sijui Mtume swalla llaahu alayhi wasallam alisoma Quraan usiku na wala sijui aliswali usiku mpaka asubuhi na wala sijui alifunga mwezi kamili isipokuwa Ramadhan.

📚SAHIH MUSLIM/746.



🍃🍃🍃🍃

Source

https://t.me/duaatsalaftz


🍂🍂🍂🌾

No comments:

Post a Comment