*📝HK Umuhimu wa kuepuka madhambi na uasi ndani ya Ramadhaan na sio tu Chakula na Kinywaji* 📝
Abu Hurayrah (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: *"Yoyote ambaye hatoacha uongo katika maneno katika maneno na kuufanyia kazi na kufanya ujinga, basi Allah Hana haja kwa yeye kuacha chakula chake na kinywaji."* Al-Bukhāri (no. 6057), Abu Dawūd (no. 2362).]
Kama ilivyotajwa hapo nyuma, maasia yanadhuru swaum. Ikiwa mtu atakuwa akifanya madhambi, funga yake ni sahihi/inaswihi lakini ujira wake unapungua au hapati ujira ya kufunga. Vitendo vibaya ni vitendo vya kimadhambi, maneno ya kimadhambi,
kutizama kimadhambi na kila kitu chochote ambacho Allah Amekiharamisha. Kwahivyo aliyefunga akianguka kwa haya makatazo yalioharamishwa hatengui sawmu yake lakini anakosa ujira (ajr), na hamna kulipiza sawmu hiyo.
Badala yake, anatakiwa atubie kwa tabia yake chafu.Uongo/Ubatili katika maneno uliotajwa katika hadith unahusisha maneno yote yaliyoharamishwa kama vile kulaani, kutukana/nyanyasa, kusengenya na Umbea.
Kwa hiyo Muislamu anawajibika kuepuka uongo/ubatili katika maneno na matendo-na kama mtu atakulaani au atakutukana, hutakiwi kujibu kwa maneno machafu, badala yake useme: *"Hakika nimefunga"* yani: funga yangu inanizuia mimi na kunilinda kutokana na aina hii ya tabia ovu. Hili limetajwa na Mtume (salallāhu ‘alaihi wasallam), *Ikiwa mtu atakutukana au mtu atakuja kupigana naye, basi na aseme: "Hakika mimi nimefunga" [Al-Bukhāri (no. 1904), Muslim (no. 1151).]*. Kwa hiyo hauwajibu watu waovu wanaozungumza kwa maneno machafu ya kimatusi-na hii inatakiwa kuwa ndio tabia ya Muislamu akiwa amefunga au la.
No comments:
Post a Comment