Sunday, 2 April 2017

Itambue Istikhaarah




Swali

Istikhaarah inaswaliwa katika mambo yote ya maisha ya muislamu au ni katika mambo muhimu peke yake?

Jibu.

Katika mambo muhimu. Mambo ya kawaida hayahitajii Istikhaarah. Unaswali Istikhaarah pale ambapo hujui kama ni bora kufanya jambo fulani au kuliacha.

🎤 Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (37)
http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%201%20...
Tarehe: 1436-10-17/2015-08-02
Toleo la: 02.12.2015
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com
[4/2, 08:20] ‪+255 714 877 821‬: *Imaam al-Fawzaan Kuhusu Du´aa Ya Istikhaarah*

Swali

Je ni bora katika Du´aa Swalah ya Istikhaarah iwe katika [ndani ya] swalah ya mwisho au baada yake [ya kutoa salam]?

Jibu

Swalah ya Istikhaarah ni kama ilivyokuja katika Hadiyth, unaswali Rakaa mbili halafu unaomba baada ya kutoa Salaam, unaomba Du´aa ya Istikhaarah.

🎤 Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan http://youtu.be/ffS_pCQ5VHg
[4/2, 08:20] ‪+255 714 877 821‬: *Swalah Ya Istikhaarah Ni Kila Anapoihitajia Mtu*

Swali

Swalah ya Istikhaarah (kumtaka Allaah ushauri/maelekezo) katika jambo, inakuwa zaidi ya mara moja au ni mara moja tu?

Jibu

Istikhaarah ni kila anapoihitajia mtu; mara moja au zaidi. Kila anapoihitajia mtu (kumtaka Allaah ushauri pale ambapo hajui kama ni bora kufanya jambo au kuliacha) anaifanya.

🎤 ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan
http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=240


[4/2, 08:20] ‪+255 714 877 821‬: *Kuomba Du´aa Ya Istikhaarah Kwa Lugha Nyingine*

Swali

Je, ni lazima Du´aa ya Istikhaarah iwe kwa lugha ya kiarabu?

Jibu

Ndio. ´Ibaadah zote zinakuwa kwa lugha ya kiarabu kwa yule mwenye kuweza hilo. Ama yule asiyeweza hilo, aombe kwa Du´aa yake.

🎤 Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/montaqo-17-10-1434_1.mp3
[4/2, 08:20] ‪+255 714 877 821‬: *Kuna Suurah Maalum Katika Swalah Ya Istikhaarah?*

Swali

Je, imethibiti kuwa kunasomwa Suurah maalum katika Swalah ya Istikhaarah?

Jibu

Sijui lolote kuhusu hili. Jambo hili ni pana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuweka Suurah maalum.

🎤 Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/montaqo-17-10-1434_1.mp3
[4/2, 08:20] ‪+255 714 877 821‬: *Kama Mtu Hakubainikiwa Na Kitu Swalah Ya Istikhaarah Anaweza Kuswali Tena?*

Swali

Baada ya kuswali Swalah ya Istikhaarah na hakubainikiwa na kitu. Afanye nini?

Jibu

Arudi kuswali Isitkhaarah. Akiswali Istikhaarah na akaomba na wala asibainikiwe na kitu, arudi kuswali mara ya pili na aombe.

🎤 ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan
http://www.youtube.com/watch?v=6tCnsG-1TOA
[4/2, 08:21] ‪+255 714 877 821‬: *Allaamah al-´Abbaad Kuhusu Wakati Wa Du´aa Ya Istikhaarah*

Swali

Du´aa ya Istikhaarah inakuwa ndani ya Swalah baada ya Tashahhud na kabla ya Salaam au baada ya Salaam?

Jibu

Inakuwa baada ya kutoa Salaam.

🎤 ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarsubject&schid=9636&subjid=3...
[4/2, 08:21] ‪+255 714 877 821‬: *Kuomba Du´aa Kwa Kunyanyua Mikono Baada Ya Swalah Ya Istikhaarah*

Swali

Je, inajuzu kunyanyua mikono kuomba Du´aa baada Swalah ya Istikhaarah?

Jibu

Ndio, akishaswali Rakaa mbili atanyanyua mikono yake na kuomba. Hakuna ubaya. Kwa kuwa kunyanyua mikono ni katika sababu za kukubaliwa (Du´aa).

🎤 Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
http://www.youtube.com/watch?v=cE8LpTf7v2o


[4/2, 08:21] ‪+255 714 877 821‬: *Kutaka Ushauri Kati Ya Wanawake Wawili Wa Kuoa*

Swali

Nina wanawake wawili ambao nimeletewa nioe. Je, niswali Swalah ya Istikhaarah kwa kila mmoja au nifanye nini?

Jibu

Inatosheleza Swalah ya Istikhaarah moja. Taka ushauri ni mwanamke yupi ambaye ni bora kwako. Huku ni kushuku baina ya mambo mawili, wanawake wawili ina ni baina ya mambo mawili.

🎤 Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/montaqo-17-10-1434_1.mp3
[4/2, 08:21] ‪+255 714 877 821‬: *Baada Ya Kuposa Msichana Ameingiwa Na Mashaka*

Swali

Nimeposa msichana mwenye Dini na baba yake amekubali na ni mtu mwema. Lakini baada ya kuposa moyo wangu umekuwa na uzito kwa posa hii bila ya sababu ninayojua. Sasa nimechanganyikiwa juu ya jambo langu. Ni ipi nasaha yako juu ya hilo?

Jibu

Swali Swalah ya Istikhaarah na Du´aa. Swali Swalah ya Istikhaarah Rakaa mbili na uombe baada yake Du´aa ya Istikhaarah.

🎤 Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg--14340505.mp3


Amesema Jaabir Bin Abdillah رضى الله عنه  “alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  akitufundisha Swala ya Istikhara kama vile anavyotufunza sura ya Qur’an.  Anasema صلى الله عليه وسلم   ‘Akikusudia mmoja wenu kufanya jambo, aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme:

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْتَخيـرُكَ بِعِاْـمِك، وَأسْتَقْـدِرُكَ بِقُـدْرَتِـك، وَأَسْـألُـكَ مِنْ فَضْـلِكَ العَظـيم، فَإِنَّـكَ تَقْـدِرُ وَلا أَقْـدِر، وَتَـعْلَـمُ وَلا أَعْلَـم، وَأَنْـتَ عَلاّمُ الغُـيوب، اللّهُـمَّ إِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ  (وَيُسَـمِّي  حاجته)  خَـيْرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، ( عَاجِلِهِ و آجِلِه)   فَاقْـدُرْهُ لي وَيَسِّـرْهُ لي ثـمَّ بارِكْ لي فيـه، وَإِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ شَـرٌ  لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، ( عَاجِلِهِ و آجِلِه) فَاصْرِفْـهُ عَنّيِ  وَاصْرِفْني عَنْـهُ وَاقْـدُرْ ليَ الخَـيْرَ  حَيْـثُ كانَ ثُـمَّ أَرْضِـني بِِـه .

“Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nakutaka ushauri (muelekezo) kwa ujuzi Wako, na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe unaweza, nami siwezi, nawe unajua nami sijui, nawe nimjuzi wa yale yaliyofichikana.   Ewe Mwenyezi Mungu  iwapo jambo hili kutokana na ujuzi wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali ) basi nakuomba uniwezeshe nilipate, na unifanyie wepesi, kisha  unibariki, na iwapo unajua kwamba  jambo hili ni shari kangu katika dini yangu namaisha yangu na mwisho wa  jambo langu (karibu na mbali) basi liepushe na mimi naminiepushe nalo, na  nipangie  jambo jengine lenye  kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo”

(Na hajuti mwenye kumtaka ushauri (muelekezo) Mwenyezi Mungu  na akawashauri waja waumini na akajidhatiti jambo lake)

(Amesema Mwenyezi Mungu  سبحانه وتعالى  kumwambia Mtume Wake صلى الله عليه وسلم

 ) وَشَاوِرْهُمْ فِي الأَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللّهِ(

(Na ushauriane nao katika mambo, na ukiazimia kufanya jambo, basi tegemea kwa Mwenyezi Mungu) Suratul Imraan: 159)



1 comment:

  1. A alykum. Swali langu Mwanamke anamatatizo ya kuchagawa.mama anasema nisimuoe kwa kuhofia nitapata shida mwanawe lakin kheri na Shari inatokana na Allah je naweza kusali swala ya istikhar kupata muangaza wa Jambo Hilo?

    ReplyDelete