Thursday, 6 April 2017

UMUHIMU WA KUSWALI SWALA KWA WAKATI WAKE NA KUWAFANYIA WEMA WAZAZI



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بن مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ الْعَمَلِ أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ؟ قَالَ: ((الصَّلاَةُ عَلَى وَقْتِهَا)) قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: ((ثُمَّ بِرُّ الْوَالِدَيْنِ)) قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟  قَالَ: ((الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd(رضي الله عنه) ambaye amesema: Nilimuuliza Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم):  ‘amali gani inayopendeza zaidi kwa Allaah? Akasema: ((Swalaah kwa wakati wake)). Akasema: Kisha ipi? Akasema: ((Kisha kuwafanyia wema wazazi wawili)). Akasema: Kisha ipi? Akasema:((Kufanya Jihaad katika Njia ya Allaah)).[1]

 MAFUNZO::::⤵⤵⤵

‘Amali zinatofuatiana kwa daraja, kwa maana kuwa nyinginezo zina thawabu zaidi ya nyingine.

 Hima kubwa ya Maswahaba kupenda kujifunza mambo ya Dini yao, kwani walikuwa wakimuuliza Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kila jambo wasilolijua.

Tabia njema ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na upole wake wa kuvumilia maswali kadhaa ya Maswahaba zake akiwajibu bila ya kuchoka.


Kuswali kwa wakati ni ‘amali bora kabisa kwa Allaah na ni amrisho katika Qur-aan.



إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ﴿١٠٣﴾



Hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu[2]



Uislamu unahimiza kuwafanyia wema wazazi wawili. [Al-Israa:  23-24, Al-Baqara: 83, An-Nisaa 4: 36, Al-An’aam 6: 151, Al-‘Ankabuut 29: 8, Luqmaan 31: 14].


 وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًاۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾


Na Mola wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu (yeyote) isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wapo akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, ‘Uff!  (neno karaha hata kunena ‘Ah!’) Na wala usiwakemee; na waaambie maneno ya heshima. Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme (kuomba): “Mola wangu! Warehemu (wazazi wangu wawili) kama walivyonilea udogoni.” [3]



Kuwafanyia wema wazazi ina thawabu zaidi kuliko kufanya Jihaad katika njia ya Allaah. [Hadiyth: ‘Abdullaah bin ‘Amr Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) alisimulia: Mtu mmoja alimkabili Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Nitakubai juu ya Hijra na kupigana Jihaad katika njia ya Allaah nikitafuta ujira kutoka kwa Allaah. Akamuuliza: ((Je katika wazazi wako yuko aliye hai?)) Akajibu: Ndio, wote wako hai. Akamuuliza: ((Unatafuta ujira kutoka kwa Allaah?)) Akajibu: Ndio. Akamwamiba: ((Rudi kwa wazazi wako na uwafanyie wema))].[4]



Mwanafunzi anatakiwa amuulize maswali mwalimu wake ambayo yatamsaidia katika dunia na Aakhirah yake.



Mwanafunzi anapaswa awe na adabu nzuri kwa mwalimu wake wala asitoke katika nidhamu hiyo ya Kiislamu.



[1]  Al-Bukhaariy na Muslim.

[2]  An-Nisaa (4: 103).

[3]  Al-Israa (17: 22-23).

[4]  Al-Bukhaariy na Muslim.

No comments:

Post a Comment